IQNA

Wahifadhi na Wasomaji Qur'ani kutoka Nchi 50 wajisajili  Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Karbala 

20:28 - April 30, 2025
Habari ID: 3480616
IQNA – Wanaharakati  wa Qur'ani kutoka nchi 50 hadi sasa wamejisajili kushiriki katika toleo la nne la shindano la kimataifa la Qur'ani huko Karbala, Iraq. 

Kituo cha Dar-ol-Qur'an cha Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) huandaa shindano hili kila mwaka, linalojulikana kama 'Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Karbala'. 

Limeandaliwa kwa kategoria za kuhifadhi Qur'ani, usomaji na tafsiri. 

Wassam Nadir al-Delfi, mkuu wa ofisi ya vyombo vya habari ya kituo hicho, amesema kuwa idadi ya waliojisajili kwa shindano hadi sasa ni 468. 

Hii inajumuisha 263 katika kategoria ya kuhifadhi, 156 katika usomaji, na 49 katika tafsiri ya Qur'ani, alisema. 

Alibainisha kuwa usajili utaisha Mei 1, na mchakato wa tathmini utaanza mara baada ya hapo. 

Amesema Misri ina idadi kubwa zaidi ya washindani (41) ikifuatiwa na Iraq (37), Iran (19), Nigeria (28), na Indonesia (20). 

Idadi hizi zinaonyesha kutambulika kwa kiwango cha kimataifa kwa tukio la Qur'ani na hadhi ya mji mtukufu wa Karbala kama kitovu cha shughuli za Qur'ani duniani, al-Delfi alieleza. 

Aliongeza kusema kuwa shindano hili ni mkusanyiko wa kimataifa wa Qur'ani kwa ajili ya kuimarisha mafungamano ya undugu na umoja wa Kiislamu chini ya mwongozo wa Qur'ani. 

Kwa kuandaa shindano hili, Astan ya Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) imecheza jukumu lake la kuhudumia Qur'ani na kuimarisha utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa vizazi mbalimbali, alihitimisha. 

Raundi ya mwisho ya toleo la nne la Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Karbala imepangwa kufanyika kwa ana huko Karbala katika tukio la Eid al-Ghadir (katikati ya Juni). 

3492889

Habari zinazohusiana
captcha